1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-Qaeda yadai kumua kamnada Mali

22 Aprili 2023

Kundi lenye itikadi kali linalohusiana na Al-Qaeda limedai kuhusika na shambulio la wiki hii ambapo mkuu wa majeshi wa Mali aliuawa.

https://p.dw.com/p/4QR8p
Symbolbild Islamisten in Burkina Faso
Picha: ROMARIC OLLO HIEN/AFP/GettyImages

Kundi lenye itikadi kali linalohusiana na Al-Qaeda limedai kuhusika na shambulio la wiki hii ambapo mkuu wa majeshi wa Mali aliuawa.Taarifa kutoka ofisi ya rais ya Mali zinasema Oumar Traore, mkuu wa majeshi katika serikali ya rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goita, ni miongoni mwa watu kadhaa waliouwawa katika shambulizi la kuvizia mnamo siku ya Jumanne karibu na mpaka wa Mali na Mauritania.Traore alikuwa miongoni mwa maafisa wa serikali walioandamana na wahandisi kutafuta maeneo ya kuchimba maji, ambao walishambuliwa takriban kilomita 400 kaskazini mwa mji mkuu Bamako.Mali imekuwa ikipambana na mzozo wa kiusalama na kisiasa tangu kuanza kwa uasi wa wenye itikadi kali na wanaotaka kujitenga kaskazini mwa Mali 2012.