1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Ajali katika mgodi wa makaa ya mawe yaua watu 12 Pakistan

20 Machi 2024

Watu 12 wamekufa nchini Pakistan baada ya kutokea maporomoko ya udongo katika mgodi wa makaa ya mawe.

https://p.dw.com/p/4dvNt
Pakistan | Mgodi wa makaa ya mawe Pakistan
Wafanyakazi katika mgodi wa makaa ya mawe PakistanPicha: Iqbal Hussain/Xinhua/IMAGO

Ajali hiyo iliyosababishwa na mripuko wa gesi ilitokea jana jioni katika mgodi wa jimbo la Khost takriban kilometa 80 mashariki mwa mji wa Quetta.

Abdul Ghani Baloch, mkaguzi mkuu wa migodi wa jimbo la Balochistan, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa juhudi za uokoaji zimehitimishwa.

Abdullah Shahwani, mkurugenzi mkuu wa sekta ya madini wa Balochistan, amethibitisha pia idadi hiyo ya vifo, huku Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif akielezea huzuni na masikitiko makubwa.

Kwa habari nyingine za ulimwengu, tazama chaneli yetu ya YouTube.