1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahueni kwa vilabu vya UIaya kuhusu AFCON

27 Desemba 2021

Siku zinaendelea kuyoyoma kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON nchini Cameroon na timu zitakazoshiriki zinaendelea kujiweka sawa na kuvitaja vikosi vyao.

https://p.dw.com/p/44s7z
Fußball Benin-Nationalspieler
Picha: Sports Inc/empics/picture alliance

Vilabu vya Ulaya hatimaye vinaweza kushusha pumzi baada ya kuruhusiwa kubaki na wachezaji wao hadi wiki ambayo tamasha hilo litaanza. Hii ni baada ya ombi la ligi za Ulaya kukubaliwa na Shirikisho la Kandanda Afrika – CAF.

Kanuni za FIFA liliwahitaji wachezaji hao wanaocheza ligi za kigeni kuruhusiwa kuondoka leo, na kurefusha muda ambao wangekosa mechi za mashindano ya Ulaya kama vile Premier League ambayo inacheza hata wakati Siku Kuu za Krismasi na Mwaka Mpya na mpaka baada ya AFCON.

Vilabu sasa vinaweza kubaki na wachezaji hao hadi Januari 3. Michuano ya AFCON itakayozishirikisha timu 24 itafungua pazia zake Januari 9 katika dimba la Olembe mjini Yaounde, Cameroon, huku fainali ikipigwa Febrauri 6.

AFP