1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afungwa miaka 11 kwa kumuua sokwe Uganda

Sekione Kitojo
30 Julai 2020

Mahakama nchini Uganda imemhukumu mwanamume mmoja miaka kumi na moja gerezani kwa kuua sokwe kiongozi aliyejulikana kama Rafiki. Sokwe huyo alitoweka na siku tatu baadaye mzoga wake ulipatikana.

https://p.dw.com/p/3gAUH
Sokwe
Picha: picture-alliance/AP Photo/WCS Nigeria

Mshtakiwa amesomewa makosa matatu ikiwemo kuua sokwe, kupatikana na nyama ya wanyamapori pamoja na vifaa vya kuwatega wanyama. Wenzake watatu wamendelea kukanusha mashtaka hayo na wamepelekwa rumande huku kesi ikiendelea.

Wahifadhi wa wanyamapori hasa wale wanaopigania kutotoweka kwa sokwe hao wa kipekee wamelezea kufurahishwa na hukumu hiyo. Mauaji ya sokwe huyo Rafiki yaliwahuzunisha watu wengi hasa waliowahi kuzuru mbuga hizo za wanyama Kusini Magharibi mwa Uganda. Kundi alilokuwa akiongoza sokwe huyo la Nkuringo ni maarufu kwa watalii wanaozuru mbuga za Wanyama za Bwindi.