1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yawaamuru wanajeshi wake Kongo kurudi nyumbani

15 Oktoba 2023

Viongozi wa jeshi la Afrika Kusini leo wamewaamuru wanajeshi wao wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kurudi nyumbani

https://p.dw.com/p/4XYMn
Afisa wa ujumbe wa MONUSCO akishika doria katika eneo karibu na Kibumba, Kaskazini mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo mnamo Janurai 28,2022
Afisa wa ujumbe wa MONUSCO akishika doria katika eneo karibu na Kibumba, Kaskazini mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya KongoPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wanajeshi hao kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono na maonevu. Wanajeshi hao wataendelea kuwepo nchini Afrika Kusini hadi uchunguzi utakapomalizika. Jeshi la Afrika Kusini limeongeza kuwa wachunguzi wamepelekwa nchini Kongo kufanya uchunguzi rasmi.

Soma pia:Tahadhari yatolewa dhidi ya MONUSCO kuondoka haraka Kongo

Linasema inasikitisha kwamba serikali yake haikuarifiwa moja kwa moja kuhusu madai hayo lakini ilifahamu kuyahusu kupitia kwenye vyombo vya habari.

Dujjaric asema ujumbe wa amani wa MONUSCO ulipokea ripoti za unyanyasaji

Mapema wiki iliyopita, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema kuwa ujumbe wa amani wa Umoja huo MONUSCO, ulipokea ripoti kwamba wanajeshi wanaodaiwa kuhusika walikuwa wakikutana baada ya saa za amri ya kutotoka nje, kwenye baa moja inayojulikana kuwa mahali ambapo ngono ya kibiashara inafanyika.