1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Afrika Kusini yauondowa ujumbe wake nchini Israel

6 Novemba 2023

Serikali ya Afrika Kusini yamuondowa balozi na ujumbe wa wanadiplomasia wake Israel, ikiwa ni hatua ya kulaani mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4YTgs
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: ESA ALEXANDER/REUTERS

Serikali ya Afrika Kusini imewaita nyumbani balozi wake na ujumbe wake wa kidiplomasia kutoka Israel, katika hatua ya kulaani mashambulizi yanayofanywa na nchi hiyo dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Afrika Kusini imeyaita mashambulio hayo kuwa mauaji ya halaiki. Serikali ya Afrika Kusini piaimetishia kuchukuwa hatua dhidi ya balozi wa Israelnchini mwake kufuatia matamshi  aliyoyatowa hivi karibuni  kuhusu msimamo wa nchi hiyo ya Afrika katika vita kati ya Israel na Hamas.

Soma pia:Wapalestina zaidi ya 10 wauwawa kwa shambulio la Israel

Hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa kuhusu matamshi ya balozi huyo wa Israel.

Waziri wa Afrika Kusini katika ofisi ya rais Khumbudzo Ntshavheni Afrika Kusini imeamuwa kuwaita nyumbani  wanadiplomasia wake wote kutoka Tel Aviv kwaajili ya mashauriano.

Waziri wa mambo ya nje Naledi Pandor ambaye leo amemkaribisha mwenzake wa Ukraine   Dmytro Kuleba,amesema wanahitaji kushauriana na wanadiplomasia hao waliokuwa Tel Aviv kutokana na hali ya mauaji ya watoto inayowatia wasiwasi katika Ukanda wa Gaza.
 

Watu zaidi ya 500 wadaiwa kuuwawa hospitalini Gaza

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW