1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yatangaza kusitisha hali ya dharura

6 Aprili 2023

Serikali ya Afrika Kusini imesitisha hapo jana hali ya dharura iliyotangazwa mwezi Februari ili kuharakisha juhudi za kukabiliana na uhaba mkubwa wa umeme.

https://p.dw.com/p/4PlmV
Afrika Kusini I Cyril Ramaphosa I
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: GCIS/AP Photo/picture alliance

Serikali ya Afrika Kusini imesitisha hapo jana hali ya dharura iliyotangazwa mwezi Februari ili kuharakisha juhudi za kukabiliana na uhaba mkubwa wa umeme. Kukatika kwa umeme kumepungua katika wiki za hivi karibuni lakini kunaendelea kuathiri shughuli za kila siku.

Afrika Kusini imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa umeme kufuatia matatizo katika shirika la umeme Eskom ambapo Waziri wa Nishati Gwede Mantashe amesema kukatika kwa umeme kunagharimu zaidi ya dola milioni 50 kwa siku kutokana na kupungua kwa uzalishaji.

Hali hiyo ya dharura ilitangazwa na Rais Cyril Ramaphosa katika hotuba yake ya kila mwaka na ilipelekea kuruhusu matumizi ya rasilimali za ziada na kuiruhusu serikali kukabiliana na vikwazo vya urasimu ili kutekeleza miradi kadhaa ya nishati.

Kulingana na makadirio ya shirika la Eskom, mgao wa umeme unatarajiwa kuendelea kwa angalau mwaka mmoja zaidi.