1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika Kusini

Afrika Kusini yalaani shambulizi la Israel mjini Rafah

28 Mei 2024

Wizara ya uhusiano wa kimataifa na ushirikiano ya Afrika Kusini, DIRCO, imeeleza kuwa nchi hiyo inaungana na jamii ya kimataifa kulaani mashambulizi ya kikatili ya Israel kwa raia wasio na hatia.

https://p.dw.com/p/4gO7I
Waziri wa mamabo ya nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor (kushoto)
Waziri wa mamabo ya nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor (kushoto)Picha: Piroschka van de Wouw/REUTERS

Nchi hiyo imesema mkondo unaochukuliwa na serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu katika vita vyake dhidi ya Hamas unahalilisha kesi yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel katika mahakama ya ICJ.

Hii ni baada ya jeshi la Israel kushambulia kambi iliyokuwa imewahifadhi Wapalestina na ambayo imeorodeshwa kuwa moja kati ya maeneo salama yaliyotengwa mahsusi kwa ajili ya wakimbizi.

Shambulio hilo limetokea siku mbili tu baada ya mahakama ya kimataifa ya haki ICJ kuiamuru Israel kusitisha mashambulizi yake mjini Rafah.