1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Afrika Kusini yaiomba China urari sawa wa kibiashara

2 Septemba 2024

China imewapokea viongozi kadha wa Kiafrika wanaoshiriki kongamano baina ya nchi hiyo na Afrika wakati ikijaribu kuimarisha uhusiano na bara hilo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali ambako imetoa mabilioni ya mikopo.

https://p.dw.com/p/4kCM6
China Beijing | Kabla ya mkutano wa kilele wa China-Afrika
Rais Cyril Ramaphosa akiwasili mjini Beijing kuelekea mkutano wa kilele wa China na Afrika, Septemba 02, 2024.Picha: Tingshu Wang/REUTERS

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pamoja na Rais wa China Xi Jinping wamekubaliana kuuboresha uhusiano wao na kuwa "ushirikiano wa kimkakati wa enzi mpya", katika ziara ya Ramaphosa nchini humo.

Xi amemwambia Ramaphosa baada ya shafla ya kumkaribisha kwamba, China itahamasisha uhusiano utakaonufaisha pande zote katika maeneo ya uchumi wa kidijitali, Akili Bandia na nishati mpya.

Soma pia: Mkutano wa kilele wa China na Afrika waanza

Ramaphosa kwa upande wake amesema Afrika Kusini iko tayari kuendelea kuwa rafiki wa kuaminika wa China.

Hata hivyo, awali alimueleza Xi kwamba alinuia kupunguza nakisi ya kibiashara na Beijing,  baada ya kushindwa kutekeleza ahadi ilizotoa kwenye mkutano uliopita ya kununua bidhaa za dola bilioni 300 za Afrika.