1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini kusambaza askari 10,000 kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

28 Oktoba 2021

Wananchi wa Afrika Kusini watapiga kura Jumatatu ijayo kuwachagua wawakilishi wao wa serikali za mitaa.

https://p.dw.com/p/42Inj

Uchaguzi huo wa Novemba Mosi unafanyika katika wakati ambao chama tawala cha ANC kinakabiliwa na shinikizo kubwa kufuatia vurugu zilizoikumba nchi hiyo zilizochochewa na hatua ya kukamatwa kwa rais wa zamani Jacob Zuma pamoja na uchumi unaoyumba kutokana na athari za janga la COVID-19. Rais Cyril Ramaphosa ameidhinisha kupelekwa wanajeshi 10,000 ili kuimarisha usalama kuelekea uchaguzi huo. Babu Abdalla amezungumza na mwandishi habari kutoka Afrika Kusini Bryson Bichwa na ambaye anaanza kwa kuelezea matayarisho ya kuelekea uchaguzi huo.