1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini kupunguza uzalishaji wa gesi chafu

Yusra Buwayhid
28 Septemba 2021

Afrika Kusini imeahidi kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, hatua iliyowafurahisha wanaharakati wa kulinda mazingira

https://p.dw.com/p/40yM7
Deutschland | Kohlekraftwerk Schkopau
Picha: Getty Images/J. Schlueter

Serikali ya mjini Pretoria hapo jana imeijuulisha ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kushughulikia mabadiliko ya tabianchi kwamba ifikapo mwaka 2025 uzalishaji wa gesi chafu hautazidi tani milioni 510 za kaboni dioksaidi na hazitapindukia zaidi ya tani milioni 420 ifikapo mwaka 2030.

Taifa hilo linaazimia kuzalisha kiwango cha chini cha gesi chafu ikilinganishwa na lengo lake la 2016 lilokuwa ni kuzalisha chini ya tani milioni 614 kwa miaka kumi ijayo. 

Hatua hiyo inategemewa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2025.