1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Afrika Kusini kufanya luteka za kijeshi na Urusi na China

Daniel Gakuba
17 Februari 2023

Afrika Kusini inaanza leo kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja na Urusi na China, hatua ambayo imeibua hofu miongoni mwa mataifa ya magharibi kuhusiana na mazoezi hayo.

https://p.dw.com/p/4NdtA
Südafrika | russische Militärfregatte Admiral Gorschkow im Hafen von Kapstadt
Picha: AFP/Getty Images

Afrika Kusini inaanza leo mazoezi ya kijeshi ya baharini pamoja na Urusi na China, hatua ambayo nchi hiyo inasema ni ya kawaida, ingawa yamezusha mashaka miongoni wa wakosoaji wanaohofu kuwa yatahujumu uhusiano na nchi za magharibi. Serikali ya mjini Pretoria imetupilia mbali hofu hizo, ikisema ilifanya pia mazoezi ya pamoja ya kijeshi na washirika wengine wa kimataifa, yakiwemo Ufaransa Novemba iliyopita. Mataifa yenye nguvu duniani yanashindana kuimarisha ushawishi wao barani Afrika, wakati mivutano kati yao ikishamiri kutoka na vita vya Ukraine na sera ya China kuelekea Taiwan. Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi za kiafrika zinazoshikilia msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mzozo wa Ukraine, na ilijizuia kulipigia kura azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka jana, la kulaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.