1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini imeanza wiki ya maombolezo

27 Desemba 2021

Afrika Kusini leo imeanza wiki ya mambolezo ya mwanaharakati wa muda mrefu dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo Askofu Desmond Tutu huku risala za rambi rambi zikitolewa kutoka kote duniani.

https://p.dw.com/p/44rS2
Anglikanische Geistliche und Menschenrechtler Desmond Tutu verstorben
Picha: Jon Hrusa/epa/dpa/picture alliance

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemtaja Tutu kuwa mtu aliyekuwa na uadilifu wa kipekee na mwanaharakati thabiti dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama pia amemtaja Tutu kuwa kielelezo bora cha maadili.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema Tutu alikihamasisha kizazi cha viongozi wa Afrika ambao walizingatia mbinu zake zisizo za vurugu katika mapambano ya uhuru.

Viongozi wa Ulaya pia wametoa rambirambi zao, Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amemtaja Tutu kuwa kiungo muhimu katika harakati za kujenga Afrika Kusini mpya na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema mapambano huyo dhidi ya ubaguzi wa rangi na mchango wake katika kulinda haki za binadamu, vitaenziwa daima.