1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yasema Afrika inahitaji kuunda silaha za taifa hilo

30 Septemba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema mataifa ya Kiafrika yangependa kuzalisha silaha katika ardhi zao badala ya kuziagiza kutoka nchini humo.

https://p.dw.com/p/4X0Tb
Spanien | Treffen der EU-Außenminister, Dmytro Kuleba
Picha: ISABEL INFANTES/REUTERS

Waziri huyo ameyasema hayo katika kongamano la kwanza la kimataifa kuhusu viwanda vya silaha unaofanyika mjini Kyiv. Maafisa kutoka zaidi ya nchi 30 na mashirika 250 ya ulinzi wanashiriki kongamano hilo, katika jitihada ya Ukraine kutaka kuimarisha sekta yake ya utengenezaji wa silaha.Akizungumza katika mkutano wa ndani, Kuleba alisema Afrika ilikuwa soko kubwa la zana za kijeshi za Ukrain, kabla taifa hilo kuingia katika vita kamili na Urusi.Amesema katika kipindi hiki ambacho Ukraine haina uwezo wa kuuza silaha yoyote kwa Afrika, nchi za Afrika zina nia ya kuzalisha silaha za Ukraine katika mataifa yao. Ukraine itagemea zaidi msaada wa kijeshi kutoka kwa mataifa ya magharibi tangu ivamiwe na Urusi.