1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa polisi auawa katika maandamano ya Kenya

31 Machi 2023

Polisi nchini Kenya imesema afisa mmoja wa polisi amefariki dunia katika mji wa magharibi mwa nchi hiyo wa Kisumu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa maandamano ya upinzani Alhamisi

https://p.dw.com/p/4PZDx
Kenia | Anti-Ruto-Proteste in Kisumu
Picha: Musa Naviye/DW

Polisi nchini Kenya imesema leo kuwa afisa mmoja wa polisi amefariki dunia katika mji wa magharibi mwa nchi hiyo wa Kisumu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa maandamano ya upinzani Alhamisi.

Soma pia: Serika ya Kenya yakataa kufanya mazungumzo na upinzani

Kifo chake sasa kinaongeza idadi ya waliofariki kutokana na maandamano hayo ya kuipinga serikali yaliyoanza Jumatatu iliyopita kufikia watu watatu.

Hapo jana polisi walikabiliana na waandamanaji mjini Nairobi na Kisumu baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuitisha maandamano kila Jumatatu na Alhamis, akimtuhumu Rais William Ruto kwa wizi wa kura katika uchaguzi uliopita na kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei unaosababisha kupanda gharama ya maisha.