1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa mkuu wa elimu Ujerumani huenda akafutwa kazi

17 Juni 2024

Waziri wa elimu wa Ujerumani Bettina Stark- Watzinger anakusudia kumfuta kazi afisa mmoja wa ngazi ya juu Sabine Döring,baada ya kutaka kulipiga marufuku kundi la wwasomi wanaounga mkono Palestina chuo kikuu Berlin.

https://p.dw.com/p/4hA7b
Ujerumani | Kamishna wa elimu Sabine Döring.
Sabine Döring ni afisa wa pili wa cheo cha juu katika wizara na anashughulikia vyuo vikuuPicha: Frederic Kern/Geisler-Fotopress/picture alliance

Wizara ya Elimu ilisema Stark-Watzinger, alituma maombo kwa kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, kumuondoa Döring ambaye ni afisa mkuu wa pili baada ya Watzinger katika wizara hiyo. 

Mapema mwezi May wanaharakati takriban 150 wanaoiunga mkono Palestina,  walitaka kuweka makambi katika chuo hicho kikuu kupinga mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza. Chuo hicho mara moja kiliwaarifu polisi kuhusu tukio hilo na mkusanyiko huo kudhibitiwa. 

Soma pia:Mkuu wa elimu Ujerumani afutwa kazi kuhusiana na majibu kwa maandamano ya Gaza

Baada ya hapo kundi la wasomi mbali mbali kutoka katika vyuo vikuu tofauti vya Berlin wakaandika barua wakiunga mkono haki ya wanafunzi kuandamana.