1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Viongozi wa Afrika wakutana kujadili mageuzi ya Umoja wa Mataifa

31 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEN7

Viongozi wa Kiafrika wanakutana leo hii kujadili repoti ya jopo la viongozi wa nchi 10 wanachama wa umoja huu juu ya msimamo Umoja wa Afrika inaopasa kuuchukuwa juu ya mageuzi ya Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa umoja huo Adam Thiam amesema Rais wa Sierra Leone Tejan Kabbah atawasilisha repoti juu ya mageuzi ya Umoja wa Mataifa katika mkutano wa dharura wa viongozi wa umoja wa Afrika unaofanyika katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa Ethiopia.

Umoja wa Afrika ulikataa kubadili madai yake ya kuwepo kwa nchi wanachama 26 wa kudumu katika baraza la uslama la umoja wa mataifa na nchi sita za wanachama wapya ziwe na uwezo wa kura ya turufu ambapo Afrika ipewe viti viwili na kuwepo na viti vengine 5 vya wanachama wa kudumu bila ya uwezo wa kura ya turufu ambapo kwayo Afrika ipatiwe viti 2.