1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ...

2 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFmz
amemteua aliyekuwa zamani waziri wa kigeni wa Canada, Lloyad Axworthy, awe mpatanishi wa ugomvi wa mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea. Naibu msemaji wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia na Eritrea, George Somewill, alisema Annan aliwaarifu kwa barua, viongozi wa Ethiopia na Eritrea juu ya kuteuliwa kwa Axworthy. Muwafaka wa amani uliotiwa sahihi na nchi hizo mbili mjini Algiers mwaka 2000 kumaliza vita vya miaka miwili vya mpaka, unakabiliwa na hatari, kwa mvutano juu ya uchoraji wa mpaka wao.