1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABAB: Ukianza mkutano wa Umoja wa Mataifa kuzungumzia maji...

9 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFtz
Afrika, Umoja wa Mataifa umetoa mwito pachukuliwe hadhari katika matumizi ya maji. Usimamizi mbaya juu ya maji unaathiri uzalishaji wa chakula, na maendeleo ya viwanda barani Afrika. Waziri wa maji wa Misri, Mahmud Abu Seid, alisistiza kwamba, asilimia 60 ya wakaazi wa vijijini Afrika hawapati maji ya kunywa, na asilimia 73 hawana vyoo. Katika mkutano huo wa siku sita nchini Ethiopia, wanashiriki mawaziri mia kadhaa wa kiafrika, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na wanasayansi.