1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA:Wafanyikazi 6 wakiwemo wajerumani 2 wa kampuni inayoihudumia kampuni kubwa ya mafuta ya Shell watekwa nyara Niger Delta,Nigeria

16 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3H

Kundi la wapiganaji katika eneo la utajiri wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria,limewateka nyara wafanyikazi wawili wakijerumani na wanne raia wa Nigeria wanaofanyia kazi kampuni moja inayotoa huduma kwa kampuni kubwa ya mafuta ya Shell.

Afisa wa kampuni hiyo amethibitisha kwamba wafanyikazi hao sita wa kampuni ya ujerumani ya B&B walitekwa nyara walipokuwa wakisafiri kwa boti huko kusini mwa nchi hiyo.

Katika eneo hilo la Delta mizozo kati ya makampuni ya mafuta kutoka nje na wapiganaji wa kikabila nchini Nigeria ni visa vinavyotokea mara kwa mara.

Eneo hilo linatoa kiasi kikubwa cha mafuta kwa wanachama wa Opec kila siku.