1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja. Wagombea waliojitoa Liberia wapongezwa.

7 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUM

Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi katika Afrika magharibi ECOWAS jana imewapongeza wagombea wa uchaguzi nchini Liberia ambao wamejiondoa katika uchaguzi mkuu wa hapo Oktoba 11 ili kuweza kuruhusu uchaguzi huo kufanyika.

Taarifa ya ECOWAS imesema kuwa inatia moyo kuona kuwa wagombea hao walioathirika wamekubali kuweka kando maslahi yao ya binafsi na kutoa umihumu kwa maslahi makuu ya kitaifa kwa kujiondoa katika kugombea nafasi katika uchaguzi huo.

Mpatanishi mkuu wa kundi hilo la mataifa ya Afrika magharibi kwa ajili ya Liberia , Jenerali Abdulsalami Abubakar , amesema siku ya Jumatano mjini Monrovia kuwa upigaji kura nchini Liberia utafanyika kama ulivyopangwa baada ya kuwashawishi wagombea kadha wa kiti cha urais kukubali kijiondoa baada ya ushindi wao dhidi ya uamuzi wa kuwaengua katika kugombania nafasi hiyo.

Uchaguzi huo kwa hiyo utafanyika kama ulivyopangwa hapo Oktoba 11.