1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja. Maendeleo ya mazungumzo ya amani kwa ajili ya jimbo la Dafur yanakwenda taratibu mno, yasema Nigeria.

26 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEzz

Nigeria siku ya Ijumaa imeelezea kutoridhishwa kwake na maendeleo madogo yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kuleta amani katika jimbo la Dafur, mazungumzo yanayofanyika mjini Abuja tangu pale yalipoanza wiki mbili zilizopita, lakini imeeleza matumaini pia kuwa sasa yatakwenda kwa haraka.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Nigeria Oluyemi Adeniji amesema baada ya kuhudhuria kikao kimoja kuwa mazungumzo hayo yanakwenda taratibu mno. Mazungumzo hayo yana lengo la kutatua tofauti kati ya makundi matatu ambayo yametia saini makubaliano ya kumaliza mzozo wa jimbo la Dafur.

Amemsifu msuluhishi mkuu katika mazungumzo hayo Bwana Salim Ahmed Salim wa Tanzania , pamoja na wasaidizi wake kwa kile alichosema kuwa ni kazi nzuri ya kujaribu kusukuma suala hilo mbele.