1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Kagame ashambulia wanasiasa kwa rushwa na ubadhirifu

23 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJ2

Rais Paul Kagame wa Rwanda hapo jana ameshambulia kile alichokiita kuwa rushwa,tamaa,umwagaji damu na ubadhirifu miongoni mwa wanasiasa barani Afrika.

Amesema katika mdahalo wa hadhara kwamba sio jambo la kutia chumvi kusema kwamba neno siasa au mwanasiasa linaendelea kubakia katika bara la Afrika kwa na maana karibu sawa na rushwa,tamaa,kujinufaisha binafsi,ubadhirifu,kujitia purukushani,upendeleo na umwagaji damu.

Amesema wao katika Afrika wanawajibika kurudisha maadili yaliopotea katika ngazi ya juu ili kwamba neno siasa liweze kuanza kuhesabiwa kuwa na kuonekana kama madaraka ya mtu na uwajibikaji wa pamoja katika kuleta mabadiliko mazuri ya kuneemesha jamii na mataifa.

Kagame alikuwa akizungumza katika semina ya tano ya kila mwaka kuhusu uhalifu wa uchumi ilioandaliwa na mashirika ya serikali yenye kuongoza vita dhidi ya tatizo hilo.