1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vilivyotokana na matetemeko Afghanistan vyafikia 2,053

8 Oktoba 2023

Baada ya kutokea matetemeko kadhaa huko magharibi wa Afghanistan, maafisa wa taifa hilo wanasema idadi ya waliokufa imeongezeka na kufikia watu 2,053.

https://p.dw.com/p/4XGXO
Afghanistan Erdbeben in Herat-Provinz
Picha: Omid Haqjoo/AP/dpa/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kabul, msemaji wa Mamlaka ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa (ANDMA) amesema kutokana na matetemeko hayo ya Jumamosi, vijiji  takribani 13 vimeteketea kabisa. Amesema zaidi ya watu 1,200 wamejeruhiwa. Idadi ya waliokufa ni ya awali kwa kuwa kazi ya uokozi bado inaendelea waokoaji. Jumamosi asubuhi katika kipindi kifupi matetemeko manane ya ardhi yalitikisa eneo la mpakani karibu na Iran.Kulingana na Shirika la Afya Duniania WHO, takriban watu 4,200 wameathiriwa na nyumba zipatazo 600 zimeharibiwa.