Viongozi kutoka Mataifa zaidi ya 100 wamewasili mjini New York kushiriki katika vikao vya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa/ Katika kuelekea uchaguzi nchini Ujerumani, vyumba vya kupiga gumzo vya Waturuki wa Ujerumani, majukwaa ya Intaneti na mitandao ya kijamii yanaeneza ushauri kuhusu namna ya kupiga kura/ Serikali ya Rwanda imeanza kuwahamisha zaidi ya wakimbizi elfu tisa wa Congo