1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi laua takriban watu 2000 Afghanistan

8 Oktoba 2023

Takriban watu 2,000 wamekufa baada ya kutokea matetemeko ya ardhi kadhaa yenye nguvu kubwa magharibi mwa Afghanistan. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa serikali ya Taliban.

https://p.dw.com/p/4XG3R
Afghanistan | Erdbeben in Afghanistan
Picha: Mashal/dpa/XinHua/picture alliance

Afisa mmoja mwandamizi katika wizara yenye dhamana ya habari na utamaduni, Abdul Wahid Rayan, amesema idadi ya waliojeruhiwa ni kubwa mno. Awali jana Jumamosi, ofisi yenye kuhusika na masuala ya dharura ya Umoja wa Mataifa, OCHA, ilisema zaidi ya watu 100 wamekufa na idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na kuwepo kwa watu waliofunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, watu wanaofikia 4,200 wameathiriwa wa tetemeko hilo na nyumba takribani 600 zimeporomoka.