1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Magenge ya uhalifu yajaribu kuvamia Benki Kuu Haiti

20 Machi 2024

Vikosi vya usalama nchini Haiti vimewauwa watu takriban watatu, na kuzima shambulio kwenye Banki Kuu ya nchi hiyo, huku ghasia za magenge ya uhalifu zikiongezeka katika viunga vya mji mkuu Port-au-Prince.

https://p.dw.com/p/4dv2O
Polisi haiti walikinda doria
Polisi haiti walikinda doria dhidi ya uvamizi wa makundi ya kihalifuPicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Benki Kuu ya Jamhuri ya Haiti BRH ni moja ya taasissi chache muhimu ambazo zilikuwa zikiendesha shughuli zake katika mji mkuu huo, ambao umezunguukwa na makundi yanayomiliki silaha kwa takriban wiki tatu sasa.

Kumeshuhudiwa majaribio kadhaa ya kuvamia bank hiyo, lakini hayakufua dafu kutokana na walinzi wa benk na polisi kuzima mashambulizi hayo.

Haiti imekumbwa na ongezeko la ghasia za magenge tangu mwishoni mwa mwezi Februari wakati makundi yenye silaha yalipovamia gereza, na kuwaachia maelfu ya wafungwa.

Soma pia:Magenge ya wahalifu nchini Haiti yaendeleza mashambulizi kwenye makazi ya watu

Wiki iliyopita Waziri Mkuu Ariel Henry alikubali kujiweka kando ili kuruhusu kuundwa kwa serikali ya mpito, kufuatia shinikizo kutoka kwa nchi jirani za Karibian na Marekani.

Viongozi wa Karibiani wamesema makundi yote na vyama vya kisiasa isipokuwa kimoja vimewasilisha wagombeaji wa baraza la mpito la rais watakaokuwa na jukumu la kuchagua waziri mkuu wa mpito Haiti.

Kwa habari nyingine zaidi, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube hapa