1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Umoja wa Mataaifa waonya juu ya hali mbaya nchini Haiti

18 Machi 2024

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto ametoa tathmini ya kutisha kuhusu hali ya machafuko nchini Haiti.

https://p.dw.com/p/4dqEB
Catherine Russell amesema watu wengi wamekumbwa na njaa na utapiamlo Haiti na kwamba Umoja wa Mataifa unashindwa kufikisha msaada wa waathiriwa.
Catherine Russell amesema watu wengi wamekumbwa na njaa na utapiamlo Haiti na kwamba Umoja wa Mataifa unashindwa kufikisha msaada wa waathiriwa.Picha: Ariana Cubillos/AP/picture alliance

Mkuu huyo wa UNICEF, Catherine Russell amesema Haiti ime kwenye hali ya kutisha ambayo haijashuhudiwa katika miongo kadhaa.

Bi Russell amesema watu wengi wamekumbwa na njaa na utapiamlo na kwamba Umoja wa Mataifa unashindwa kufikisha msaada wa watu wa Haiti, kutokana na magenge kukidhibiti sehemu kubwa za mji mkuu wa Port-au-Prince pamoja na barabara kuu zinazoelekea kwenye miji mingine.

Ripoti ya hivi majuzi ya Umoja wa Mataifa imesema kutokana na kuwepo serikali dhaifu nchini Haiti, huduma za kimsingi zinakaribia kuporomoka nchini humo. Nchi hiyo pia inakumbwa na ukame na majanga ya asili.