1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe yakabiliwa na ukame mkubwa

26 Agosti 2016

Zimbabwe ambayo zamani ilifahamika kama mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika inakumbwa na ukosefu mkubwa wa maji ambao unaweza kusababisha na ukame wakati nchi hiyo ikiwa inaelekea katika kipindi cha kiangazi.

https://p.dw.com/p/1JqGv
Kijana akichota maji katika mto baada ya kumaliza kuogaPicha: AP

Kutokana na ukosefu wa maji, wananchi nchini Zimbabwe sasa wanatembea mpaka umbali wa kilometa 15 kufatuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kunywesha mifugo yao kutokana na vyanzo vingi vya maji kukauka, yakiwemo mabwawa na visima.

Wafugaji na wananchi wa kawaida wanapata wasiwasi kuhofia mifugo yao kufariki na wao kukosa maji ambapo kwa sasa maji hupatikana katika kisima kimoja tu ambacho hutegemewa na kaya zaidi ya 100 na kila familia hupata wastani wa ndoo mbili za lita 20 kwa siku.

Miezi michache iliyopita Zimbabwe ilikubwa na El-Nnino ambayo ilisababisha ukame uliowasababishia takribani watu milioni 4.5 kukabiliwa na ukosefu wa chakula hii, kwa mujibu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP.

El-Nino hiyo ambayo ilikuwa ni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 35 illisababisha ukame mkubwa, joto na ukosefu wa maji nchini Zimbabwe.

Cholera Epidemi in Simbabwe
Wanawake na watoto wakisubiri maji mjini HararePicha: AP

James Jofirisi mkaazi wa maeneo ya vijijini anasema kumekuwa na uhaba mkubwa wa maji na hata bwawa ambalo hutumika linaweza kukauka muda wowote.

Misaada ya wahisani inahitajika

Katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya simu na waziri wa masuala ya wanawake, jinsia na maendeleo nchini humo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuongeza kuwa Zimbabwe haina suluhisho la tatizo hilo zaidi wanategemea misaada ya wahisani

Nae waziri wa fedha nchini humo Patrick Chinamasa amesema serikali inaweza kusaidia kwa kutoa fedha kupitia mifuko ya maendeleo ya wilaya ili kufanya ukarabati wa visima visivyofanya kazi na kuchimba visima vipya hasa maeneo ya vijiji pamoja na kuwa hajaweka wazi zoezi hilo linaweza kugharimu pesa kiasi gani.

Zimbabwe ni moja kati ya nchi ambazo ziliathiriwa zaidi na El-Nino hasa katika maeneo ya Manicaland, Masgingo, Mertebeleland kusini na kaskazini

Mwandishi: Celina Mwakabwale/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef