1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Zimbabwe kuyachunguza madai ya kashfa ya 'Gold Mafia'

4 Aprili 2023

Serikali ya Zimbabwe imesema itachunguza madai ya ubadhirifu na rushwa yaliyoibuliwa na filamu fupi kuhusu ulanguzi wa dhahabu na utakatishaji fedha nchini humo, Gold Mafia.

https://p.dw.com/p/4Pglp
Simbabwe führt Goldmünzen als Zahlungsmittel ein
Picha: Tsvangirayi Mukwazhi/AP/picture alliance

Filamu hiyo ya sehemu nne za uchunguzi wa kiuandishi uliofanywa na shirika la utangazaji la Al Jazeera unadai magenge yenye mafungamano na maafisa wa serikali wanatumia uuzaji dhahabu nje ya nchi kutakatisha fedha chafu.

Waziri wa habari wa Zimbabwe Monica Mutsvangwa ameuambia mkutano wa waandishi habari kwamba serikali inayachukulia madai yaliyo katika filamu hiyo kwa uzito mkubwa na imeziamuru idara husika zianzishe uchunguzi.

Waziri huyo pia amesema atakayekutwa amejihusisha na vitendo vya rushwa, ubadhirifu au aina yoyote ya uhalifu atakabiliwa na nguvu kamili ya mkono wa sheria.