1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky: Wanajeshi wanazingatia sheria za kiutu vitani

15 Agosti 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wanajeshi wake wanazingatia kwa umakini mkubwa sheria ya kiutu na mikataba ya kimataifa katikati ya vita na Urusi

https://p.dw.com/p/4jTdS
Wanajeshi wa ukraine katika Jimbo la Sumy
Wamajeshi wa Ukraine wakiendesha kifaru kilichotengenezwa Urusi cha T-72. katika eneo la Sumy karibu na mpaka wa Urusi, Agosti 12, 2024Picha: Roman Pilipey/AFP/Getty Images

Rais Zelenskyy amesema suala hilo tayari lilijadiliwa kwenye mkutano na viongozi wa Ukraine lakini pia misaada wa kiutu imeandaliwa kwa ajili ya raia walioko kwenye eneo kubwa la Ukraine linalodhibitiwa na Urusi.

Rais huyo wa Ukraine amesema wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wanaweza kuruhusiwa kuingia kwenye maeneo hayo ili kufanya tathmini.

Maafisa wa Ukraine wamesema, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa yanayotoa misaada ya kiutu yanaruhusiwa kuingia kwenye eneo la Kursk linalokaliwa na Ukraine.