1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR:Mkutano kati ya makatibu wakuu wa CCM na CUF kufanyika

30 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWJ

Makatibu wakuu wa chama tawala cha CCM bwana Phillip Mangula na Maalim Seif Sharif Hamadi wa chama cha upinzani cha wananchi Zanzibar CUF watakutana hii leo jioni kwenye hoteli ya Bwawani kujadili hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu visiwani humo.

Viongozi wa dini mbali mbali jana usiku walikutana na wagombea wote wa bunge na Urais visiwani Zanzibar wa uchaguzi mkuu ujao.

Viongozi hao wamewawaomba wagombea wote wawasihi wafuasi wao wazingatie amani na wakomeshe uhasama wa kisiasa uliozagaa visiwani humo.

Kumefanyika sala maalum pemba za kuombea amani na utulivu leo hii.

Hatua ya viongozi wa kidini imekuja baada ya kuona machafuko ya kisiasa yanaendelea visiwani humo ambapo utumiaji wa Mawe,Mapanga na Mitarimbo umeanza dhidi ya wafuasi wa vyama vingine vya kisiasa.