1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar yakataliwa uanachama wa FIFA

Ramadhan Ali31 Oktoba 2005

Zanzibar yakataliwa uanachama wa FIFA na yapigwa kumbo nje ya CAF-shirikisho la dimba la Afrika. Duru ya kwanza ya Kombe la klabu bingwa barani Afrika kati ya Etoile na Al Ahly yamalizika suluhu 0:0 mjini Sousse, Tunesia. Na mwishoe, Kenya na mashindano ya ubingwa wa ndondi ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/CHYU
Michael Ballack
Michael BallackPicha: picture-alliance/dpa

Na Bundesliga-Ligi ya Ujerumani:

Michael Ballack alibainisha jumamosi kwanini Bayern Munich inamn’gan’gania asiache mkono, kwani yeye tena aliewapatia bao la ushindi dhidi ya FC Cologne.Munich ilikandika Cologne mabao 2:1.ilikua Cologne lakini ikicheza nyumba ni iliotangulia kutia bao kabla Ballack kutia bao la kichwa mnamo dakika ya 80 ya mchezo na kuondoka na pointi 3.Ilikua pia Ballack aliwapatia Munich bao pekee la ushindi kati ya wiki katika kinyan’ganyiro cha Kombe la Shirikisho.

Werder Bremen imebakia nafasi ya pili nyuma ya Munich baada ya kuirarua Eintracht Frankfurt kwa mabao 4-1.Hamburg inafuiata nyuma ya Bremen kwa kuishinda Schalke bao 1:0.

Klabu 3 zinaburura mkia wa Ligi-Nuremberg;Kaiserslauten na Duisburg. Kwani, jana Mainz iliitandika Nuremberg mabao 4-1.

Katika duru ya kwanza ya finali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika,Etoile Sahel ya Tunisia ikicheza nyumbani, ilimudu kutoka suluhu tu 0:0 na Al Ahly ya Misri .Al Ahly, mabingwa mara tatu wa Kombe hili wana kila nafasi sasa ya kumaliza udhia nyumbani Cairo hapo novemba 12 na kutwaa kombe la Afrika la klabu bingwa kwa mara ya 4.Mshindi ataiwakilisha Afrika katika finali ya Kombe la dunia la klabu bingwa mjini Tokyo,Japan hapo Desemba.

Ivory Coast itakayoshiriki kwa mara ya kwanza katika Kombe la dunia hapa Ujerumani mwakani,itacheza mpambano wa kirafiki na mabingwa mara tatu wa dunia-Itali mjini Geneva,Uswisi mwezi ujao.Huu utakua mpambano wa kwanza kabisa kwa timu hizo mbili kukutana hapo nov.16.Utakua mpambano wa kwanza pia kwa tembo wa Ivory Coasttangu kukata tiketi yao ya Kombe la dunia baada ya kuizaba Sudan mabao 3-1.

Ivory Coast iliwahi kupambana mara 2 tu na timu za Ulaya.Iliilaza Uswisi bao 1:0 1983 na ikalazwa na Ufaransa 3-0.Afrika Kusini inapanga kutangaza mwaka ujao viwanja vitakavyoaniwa kombe la dunia la kwanza barani Afrika hapo 2010.

Dany Jordaan,kiongozi wa Kamati ya maandalio ya kombe la dunia ya Afrika Kusini anapanga kutangaza viwanja 10 na viwanja 13 vilivyotajwa awali vingali vikizingatiwa ili mwishoe kutoa orodha ya viwanja hivyo 10.

Viwanja hivyo 13 vya awali ni Johannesberg,Pretoria,Bloemfontein,Cape Town,Durban,Kimberly,Nelspruit,Polokwane,port Elizabeth na Orkney.

Morocco iliopigwa kumbo nje ya Kombe lijalo la dunia na Tunesia, imejipatia kocha mpya nae ni mfaransa Philippe Troussier.Amefunga mkataba wa miaka 4 na shirikisho la dimba la Morocco.

Troussier aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa za Afrika:Afrika Kusini,Nigeria,Ivory Coast,Burkina Faso na hata Qatar na Japan.

Zanzibar mwishoni mwa wiki sio tu imegonga vichwa vya habari kwa uchaguzi,bali hata katika medani ya spoti ulimwenguni: FIFA imeikatalia Zanzibar uanachama.Utakumbuka timu ya Taifa ya Zanzibar-Zanzibar Heroes ilikuja hapa Ujerumani hapo Mei kujitembeza kuwa mwanachama wa FIFA baada ya CAF-shirikisho la dimba la Afrika kuipa uanachama.