1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar. Uchaguzi kufanyika zanzibar, bara waahirishwa.

29 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CENl

Tanzania imeahirisha uchaguzi mkuu wa rais na bunge siku ya Alhamis, uchaguzi uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili , baada ya kifo cha mgombea wa chama cha upinzani , lakini uchaguzi huo katika visiwa vya Zanzibar unaonekana kuwa utaendelea kama ulivyopangwa.

Jumbe Rajab Jumbe, mwenye umri wa miaka 65 ambaye ni mgombea mwenza wa chama cha tatu kwa ukubwa nchini Tanzania , Chadema , alifariki dunia siku ya Jumatano usiku kwa ugonjwa wa mshituko wa moyo, na kusababisha maafisa wa tume ya uchaguzi kufanya kikao cha muda mrefu kuamua iwapo uchaguzi huo uahirishwe ama la.

Uchaguzi huo katika eneo la Tanzania bara utafanyika hapo Desemba 18, kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Louis Makame.