1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR. Tume ya uchaguzi nchini Zanzibar yatangaza matokeo

1 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEMq

Tume ya uchaguzi nchini Zanzibar imetangaza rasmi matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Tume hiyo ya uchaguzi imetanzagaza kwamba chama tawala cha CCM kimeshinda viti vya baraza la wawakilishi 27 huku chama kikuu cha upinzani cha CUF kikijipatia viti 19.

Maelfu ya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha CUF kisiwani Zanzibar wamejazana katika makao makuu ya chama hicho na kukataa amri ya polisi ya kuwataka waondoke kutoka mahala hapo.

Leo ni siku ya tatu ambapo walinda usalama wamelazimika kutumia vitoa machozi na magari ya kumwaga maji ili kuwatawanya wafuasi wa upiunzani ambao wanadai ushindi wa chama chao katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Mbali na fujo na ghasia zilizokumba uchaguzi wa Zanzibar, asilimia 80 ya watu walijitokeza kupiga kura zao.