1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR: Polisi wafyetua risasi katika umati

9 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CETS

Viongozi wa upinzani kisiwani Zanzibar wamesema kuwa polisi wa kuzuia ghasia wamewapiga risasi si chini ya wafuasi 19 wa upande wa upinzani, waliojaribu kuvuka vizuizi vya barabarani na kwenda kuhudhuria mkutano wa hadhara.Hakuna mtu alieuawa lakini zaidi ya watu 48 walijeruhiwa vibaya katika machafuko yaliotokea huku uchaguzi wa Oktoba 30 ukijongea.Lakini mkuu wa uchunguzi wa uhalifu kiswani Zanzibar,Ramadhani Kinyogo amesema,watu 8 walipigwa risasi baada ya kupinga amri za polisi za kuwazuia kukusanyika mahala pa mkutano wa kampeni ya uchaguzi,kufuatia ripoti kuwa kutatokea machafuko.Kwa wakati huo huo,mkuu wa polisi katika kanda ya kaskazini,Khamis Kheri amesema,polisi walitumia gesi ya machozi kulitawanya kundi la wafuasi wa upande wa upinzani waliojaribu kukivamia kituo cha polisi na kumrushia mawe afisa mmoja.Ripoti za mashahidi zinasema kuwa polisi walifyetua risasi,gruneti za kuduwaza na gesi ya kutoa machozi katika umati wa wafuasi wa upande wa upinzani wapatao mia kadhaa kaskazini ya Stone Town.Mpiga picha wa Shirika la habari la AFP aliekuwepo eneo hilo amesema,polisi walifyetua kati ya rauni 20 hadi 30 za gesi ya machozi na gruneti za kuduwaza.