1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR: Hotuba za wabunge kwanza zipitiwe na spika

2 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPo

Wanachama wa chama kikuu cha upinzani kisiwani Zanzibar siku ya Jumanne walitoka nje wakati wa kikao cha bunge,baada ya mbunge wa upinzani kukatazwa kusoma hotuba ambayo hapo kabla haikuhakikiwa na spika wa bunge.Mwezi uliopita, wabunge waliarifiwa na spika Pandu Ameir Kificho kupeleka hotuba zao katika ofisi yake kuhakikiwa kabla ya kuzisoma bungeni,ili kuzuia kile alichokiita”matamshi ya uchochezi yanayoweza kusababisha mvutano.”