Zaidi ya watu 100,000 wakimbia makaazi yao Kongo
8 Januari 2025Matangazo
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, baina ya tarehe 1 na 3 Januari, mapigano makali kati ya jeshi na waasi wa M23 katika mji Masisi Kati, jimbo la Kivu Kaskazini, yamewahamisha makwao watu 102,000.
Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda inadai kuwa eneo lililotwaliwa na waasi wa M23 hivi karibuni lilikuwa kwenye mikono ya wanamgambo wa Kihutu, FDLR, wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.
Soma zaidi: Wanne wauawa, 25 wajeruhiwa kwa mabomu ya M23
Kwenye taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, alilaani ukosoaji wa jamii ya imataifa ambayo alisema haikuwahi kulaani kuvamiwa kwa mamlaka ya ardhi ya Kongo inayomililiwa na jamii za Wakongo, wakiwemo Watutsi wa Kikongo.