1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yi: Mwelekeo wa mkutano wa Xi-Biden si rahisi

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kwamba mwelekeo wa mkutano kati ya rais Xi Jinping na Joe Biden sio "rahisi." Wang ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ya nadra mjini Washington.

https://p.dw.com/p/4YAJl
Waziri wa mambo ya Nje wa China Wang Yi akizungumza na mwenzake wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa mambo ya Nje wa China Wang Yi akizungumza na mwenzake wa Marekani Antony Blinken.Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Katika ziara yake hiyo Wang alikutana na rais Biden na maafisa wengine wa ngazi za juu Marekani na pande zote kukubaliana kuandaa mkutano wa kilele kati ya viongozi wa nchi hizo mbili mwezi ujao wa Novemba.

Wang alisema Jana Jumamosi kwamba pande zote mbili zinatumai kuleta utulivu na kuboresha uhusiano wa nchi mbili haraka iwezekanavyo na kukubaliana kufanya kazi pamoja kuelekea mkutano wa kilele wa San Francisco kati ya wakuu hao wawili wa serikali zao.

Soma pia:Blinken, Wang wakutana kwa siku ya pili Marekani

Rai Joe Biden amemwalika Xi mjini San Francisco mwezi Novemba, kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) wakati uhusiano wa mataifa hayo mawili yenye nguvu ukizorota. Xi bado hajathibitisha uwepo wake.