Yemen yakabiliwa na hatari ya 'kuporomoka' zaidi
31 Mei 2017Katika kikao cha baraza la Umoja huo naibu katibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kibinadamu Stephen O Brien alisema hali iliyoko sasa imesababishwa na vitendo vya wapiganaji wanaomuunga mkono rais wa zamani na waasi wa kishia wa Houthi,.Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa watu millioni 17 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula nchini Yemen ikiwa ni pamoja na wengine millioni 6.8 walio katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa. Taifa hilo maskini la kiarabu, tangu Septemba mwaka 2014 limeandamwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya waasi wa Houthi kuuteka mji mkuu sanaa na kumwondoa madarakanai rais Abed Rabbo Mansour Hadi ambae serikali yake ilikuwa tayari ikitambuliwa na jamii ya kimataifa.Naibu katibu Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kibinadamu Stephen O Brien amesema ni swala la kuhuzunisha kuwa raia wa Yemen wanakabiliwa na magonjwa mbalimbali na wengine kufariki huku ulimwengu ukitazama. “Hili si swala ambalo halikutazamiwa .Ni matokeo ya moja kwa moja ya hatua za wahusika na wanaunga mkono mgogoro Yemen.Hayo yote pengine yametokana na tofauti zilizopo katika jamii ya kimataifa.alisema O'Brien.Mwezi Marchi mwaka 2015,muungano unaongozwa na saudi Arabia na kuungwa mkono na Marekani ulianzisha kampeini dhidi ya waasi wa Kihouthi wanaomuunga mkono rais aliyepinduliwa Ali Abdullah Saleh, ili kusadia kurejea serikali inayotambuliwa na jamii ya kimataifa ya Manosur Hadi.Tangu wakati huo waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na taifa la Iran wametimuliwa katika maeneo mengi ya kusini mwa Yemen ,lakini bado wanaudhibiti mji mkuu Sanaa na sehemu kubwa ya kaskazini. Mwakilishi wa Umoja wa mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed amesema vurugu hasa zinaendelea sehemu mbalimbali nchi humo,lakini zimeongezeka pwani ya magharibi ambako vikosi vya serikali vinajaribu kupiga hatua kuelekea bandari ya Hodeida na pia mji wa Taiz.Kutokana na hali hiyo Naibu Katibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kibinadamu Stephen O Brien ana ombi hili "Naziomba nchi wanachama kuhakikisha juhudi zote zinafanywa ili kuiweka bandari ya Hodeidah wazi na undeshaji wake kuendelea kama kawaida.Mashambulizi dhidi ya bandari ya Hodeidah si kwa maslahi ya upande wowote , kwasababu moja kwa moja yatawatumbukiza raia wa Yemen katika baa la njaa.alisema naibu katibu huyoKundi la mashirika 22 ya kimataifa ,na masharika mengine yanayotoa misaada ya kiutu nchini Yemn yalitaka baraza la uslama laUmoja wa matifa kuchukua hatua na kumaliza mapigano hayo yaliyockua muda mrefu.
Mwandishi:Jane Nyingi
Mhariri:Yusuf Saumu