1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yellen aikosoa China kwa kuzikandamiza kampuni za Marekani

7 Julai 2023

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen ametoa wito wa kufanyika mabadiliko katika soko la China. Ametoa wito huo katika siku ya pili ya ziara yake mjini Bejing, inayolenga kupunguza msuguano kati ya madola hayo makuu.

https://p.dw.com/p/4TZ7O
US-Finanzministerin Yellen in China
Picha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance/dpa/

 Akizungumza mjini Beijing, Yellen ameikosoa nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani kwa hatua zake kali za hivi karibuni dhidi ya kampuni za Marekani, na hatua mpya ya kukagua madini muhimu yanayoelekea Marekani.

Yellen ambaye aliwasili beijing hapo jana Alhamis, amesema hatua hizo zinaonyesha haja ya kuwepo kwa mifumo thabiti ya usambazaji bidhaa na akaonya kwamba Marekani na wandani wake, watajibu kile alichokiita "vitendo vya kiuchumi visivyo sawa."

Ziara hiyo ya Yellen ni sehemu ya ziara kadhaa zenye lengo la kutuliza mivutano kati ya Marekani na China. Baadae leo anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang.