YANGON : Wito wa kuachiliwa kwa Suu Kyi
20 Juni 2005Matangazo
Wapinzani wa utawala wa kijeshi wa Burma hapo jana wameadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwa kiongozi wa upinzani aliyoko kizuizini Aung San Suu Kyi kwa maandamano barani kote Asia ikiwa ni pamoja waandamanaji 500 katika mji mkuu wa Myanmar.
Mjini Washington Rais George W Bush wa Marekani amewataka magenerali wanaoitawala nchi hiyo kumuachilia huru mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel kutoka kifungo cha nyumbani na kuheshimu matokeo ya uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika hapo mwaka 1990.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan pia ametowa wito wa kuachiliwa kwa Suu Kyi.
Mama huyo amekuwa gerezani au kwenye kifungo cha nyumbani kwa miaka 9 katika kipindi cha miaka 16 iliopita.