Wengi wetu hufurahia jua na kulalamika juu ya mvua. Lakini joto linapokuwa kali, tunaikumbuka mvua. Tangu Juni mwaka huu maeneo kadhaa duniani yamekabiliwa na wimbi la joto kali, ambalo limesababisha maafa makubwa kama vile mioto, kuharibu mazao na vifo. Karibu katika makala ya mtu na mazingira ikisimuliwa naye Sylvia Mwehozi.