1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yaomba msaada wa haraka wa vifaa tiba Gaza

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema leo kwamba takriban watu 22,500 katika Ukanda wa Gaza unaokabiliwa na vita wanahitaji huduma maalum za matibabu.

https://p.dw.com/p/4kYry
Mtoto akipokea matibabu eneo la Ukanda wa Gaza
Mtoto akipokea matibabu eneo la Ukanda wa GazaPicha: Hani Alshaer/Anadolu/picture alliance

Kulingana na tathmini ya WHO, mahitaji makubwa ya matibabu, sehemu za bandia za mwili na vifaa vya kusaidia kutembea havipatikani vya kutosha.

Mwakilishi wa Shirika la Afya katika Ukanda wa Gaza, Richard Peeperkorn, amesema wanahitaji msaada kwa haraka hasa vifaa tiba vya kukarabati miili ya watu na kwamba hawawezi kusubiri mpaka makubaliano ya kusimamisha vita yatakapofikiwa. 

Soma pia:Watu 18 wameuwawa baada ya Israel kushambulia shule katikati mwa Ukanda wa Gaza
WHO, imesema wagonjwa wengi wanaohitaji ukarabati wameumia viungo na kwamba kati ya watu 3000 hadi 4000 wamekatwa viungo tangu vita vilipoanza katika Ukanda wa Gaza. Kulingana na shirika hilo, tatizo hilo la uhaba wa vifaa tiba muhimu na madaktari ni mambo yanayoongeza shida kwa watu wa Gaza.