1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO kufanya chanjo ya Ebola, DRC

15 Mei 2018

Shirika la afya duniani WHO limepewa idhini na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuingiza na kutumia chanjo ya majaribio ya kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini humo.

https://p.dw.com/p/2xkuH
Ebola-Ausbruch im Kongo
Picha: Reuters/J. R. N'Kengo

Shirika la afya duniani WHO limepewa idhini na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuingiza na kutumia chanjo ya majaribio ya kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini humo. Mkurugenzi mkuu wa WHO Dokta Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia wanahabari kuwa sasa wana idhini ya kutumia chanjo hiyo na kuipongeza serikali ya Congo kwa kuchukua hatua za haraka kuudhibiti ugonjwa huo, ambao umewaua watu 19 hadi sasa. Wiki iliyopita, WHO iliripoti kuwa Ebola imezuka katika eneo la Bikoro lililoko katika jimbo la Equateur. Takriban watu 393 wanafuatiliwa kuona kama waliambukizwa virusi hivyo na walioathiriwa ni 39.