1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP lasitisha harakati Ukanda wa Gaza

29 Agosti 2024

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kusitisha harakati za wafanyakazi wake katika Ukanda wa Gaza baada ya gari lake kufyatuliwa risasi kwenye kituo cha ukaguzi cha jeshi la Israel.

https://p.dw.com/p/4k2Oz
Welternährungsprogramm der Vereinten Nationen
Picha: Sascha Steinach/dpa/picture-alliance

Mkuu wa shirika hilo Cindy McCain, amesema tukio hilo halikubaliki kabisa na ni la hivi punde zaidi katika mfululizo wa matukio yasiyo ya lazima ambayo yamekuwa yakihatarisha maisha ya wafanyakazi wa WFP huko Gaza.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kuwa gari hiyo ililengwa na askari wa Israel Jumanne usiku na waliifyatulia risasi 10 ambazo baadhi zililenga kioo cha mbele cha gari hiyo. Hata hivyo hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.