1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, yupo Slovenia

5 Desemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, amewasili leo nchini Slovenia kwaajili ya mazungumzo kuhusu mpango wa kuongeza wanachama katika Umoja wa Ulaya

https://p.dw.com/p/4ZoLf
Slowenien Ljubljana 2023 | PK Außenministerinnen Baerbock & Fajon
Picha: Florian Gaertner/photothek/picture alliance

Pamoja na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Kabla ya kuwasili Slovenia waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani, alibaini kwamba mapambano dhidi ya mgogoro wa mabadiliko ya tabia nchi ni kitisho kikubwa kwa usalama wa binadamu na kwamba utekelezaji wa mpango kati ya Ujerumani na Slovenia utaanza kwa kulitazama hilo. Baadae Baerbock ambaye ni mwanasiasa wa chama cha kijani nchini Ujerumani, amepangiwa kukutana na waziri mkuu Robert Golob na waziri wa mambo ya nje Tanja Fajon katika mji mkuu wa Slovenia, Ljubljana. Mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita zaidi katika suala la kuzijumuisha nchi za Balkan katika Umoja wa Ulaya kufuatia vita vya Urusi na Ukraine.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW