1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani kuitembelea Israel

7 Januari 2024

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock anafanya ziara ya nne Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4ax71
Israel Tel Aviv | Annalena Baerbock, deutsche Außenministerin | Pressekonferenz
Annalena Baerbock, waziri wa mambo ya nje wa UjerumaniPicha: Joseph Campbell/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametoa wito wa kukomeshwa machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati kabla ziara yake ya nne katika eneo hilo tangu mashambulizi ya Oktoba 7 mwaka uliopita kutoka Ukanda wa Gaza. Baerbock amesema ugaidi lazima ufike mwisho, mahitaji ya kiutu ya wakaazi yashughulikiwe na eneo la Mashariki ya Kati liondokane na mzunguko wa machafuko ya umwagaji damu kabla kuondoka Berlin kuelekea Israel.

Baerbock anatarajiwa kukutana na Rais wa Israel Isaac Herzog na Waziri wa Mambo ya Nje, Israel Katz. Baerbock amesema huku Israel ikiwa na haki ya kujilinda yenyewe kutokana na ugaidi, raia sharti walindwe vyema zaidi wakati wa harakati za kijeshi. Baerbock aidha ametoa wito msaada wa kibinadamu uongezwe katika Ukanda wa Gaza kukabiliana na njaa, magonjwa na baridi.