1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Waziri wa mambo ya nje wa Saudia ziarani Syria

18 Aprili 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Saudia Faisal bin Farhan Al Saud, anatarajiwa kuwasili mjini Damascus, mji mkuu wa Syria katika ziara ya kwanza kufanywa na afisa wa Saudi Arabia nchini Syria tangu kufumuka kwa vita nchini humo

https://p.dw.com/p/4QEEN
Saudi Arabien | Faisal bin Farhan bin Abdullah trifft Faisal Mekdad in Dschidda
Picha: SAUDI PRESS AGENCY/REUTERS

Katika miezi ya hivi karibuni, viongozi wa nchi kadhaa za kiarabu, wamekuwa wanasogea kwa rais Bashar al-Assad wa Syria ambaye hapo awali alitengwa kisiasa tangu kuanza kwa mgogoro wa nchini mwake.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan anafanya ziara nchini Syria muda mfupi tu baada ya waziri wa mambo ya nje wa Syria Faisal Mekdad kufanya ziara nchini Saudi Arabia.

Soma pia: Mataifa ya Kiarabu yaujadili mgogoro wa Syria

Kwenye mkutano wao mawaziri hao walijadili njia zinazolazimu kuchukuliwa ili kuondosha kutengwa kwa Syria. Wiki iliyopita viongozi wa nchi za kiarabu walikutana kwenye mji wa Saudi Arabia wa Jeddah kujadili njia za kuumaliza muda  mrefu wa kutengwa kwa Syria kidiplomasia.

Saudi Arabia ilivunja uhusiano wa kibalozi na Syria mnamo mwaka 2012 na pia iilisimama mstari wa mbele katika harakati za kutaka kuangushwa utawala wa Assad.