1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIreland

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak yuko mjini Belfast

28 Februari 2023

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak yuko Belfast kuanza kuipigia debe mipango mipya ya biashara baada ya mkataba wa Brexit, aliyotiliana saini na Umoja wa Ulaya, akilenga kupata uungaji mkono wa vyama vya wafanyakazi

https://p.dw.com/p/4O4Mv
Großbritannien London | Rishi Sunak
Picha: Tayfun Salci/ZUMA Press/picture alliance

Sunak alifikia makubaliano na Umoja wa Ulaya jana ili kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya Ireland Kaskazini na Uingereza na kuwapa wabunge nguvu zaidi kuhusu kanuni na sheria wanazozifuata kutoka Umoja wa Ulaya.

Muafaka huo unalenga kutatua mivutano iliyosababishwa na itifaki ya Ireland Kaskazini, makubaliano magumu ambayo yaliweka sheria za kibiashara kwa mkoa huo ambao ni himaya ya Uingereza na ambazo London iliridhia kabla ya kujuiondoa katika Umoja wa Ulaya lakini sasa inasema haziwezi kutekelezeka. Viongozi wa Umoja wa Ulaya na wa Uingereza wamesifu makubaliano hayo waliyoyasaini jana, kuhusu utaratibu wa biashara kati ya Ireland na Ireland Kaskazini, baada ya mwaka mzima wa malumbano na kuhasimiana kisiasa.